Moja ya aina ya story zinazovutia watu wengi ni pamoja na
story ambazo zina matukio ya ajabu ama matukio ambayo yako tofauti na watu walivyozoea.
Kutoka Zimbabwe kulikuwa na story ambayo ilikaa kwenye
headlines sio za Zimbabwe tu, ila duniani kote; ishu ya Rais wa nchi hiyo
kuanguka wakati akishuka ngazi.
Leo nakupa hii nyingine ya jamaa ambaye amejikuta akiangukia
kwenye mikono ya hakimu wa Mahakama na kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela
kwa kosa la kula nyama ya chatu !.
Jamaa huyo, alijitetea kwamba mara nyingi amekuwa akila
nyama hiyo ili kutibu maradhi ya uti wa mgongo na imekuwa ikimsaidia kwa kiasi
kikubwa sana, utetezi ambao Mahakama haikuonekana kuujali.
Katika upelelezi wa Polisi walikuta ngozi ya chatu
iliyokaushwa pamoja na nyama ndan ya nyumba ya Maramba
Hukumu hiyo imetokana na jamaa huyo kuonekana akikiuka
sheria ya uhifadhi wa chatu, ambao ni sehemu ya viumbe ambavyo vinatakiwa
kuhifadhiwa na kulindwa
