Social Icons

Tuesday, December 16, 2014

Ile issue ya Escrow, hii ni taarifa ya Kiongozi mmoja kujiuzulu leo December 16

Wiki chache zilizopita wakati Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea, macho ya watu wengi na masikio yalikuwa na hamu ya kutaka kuujua mwisho wa sakata la Escrow.
Wakati watu wengi wakisubiri maamuzi yatakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuhusiana na Ripoti juu ya issue ya ubadhilifu wa fedha kwenye akaunti ya Escrow, leo December 16 kuna taarifa iliyotufikia muda mfupi iliopita kuhusu kiongozi mmoja wa Serikali kujiuzulu.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV inasema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu siku ya leo na barua yake tayari imefika Ikulu ambapo Rais Kikwete ameridhia maamuzi hayo na kumshukuru kwa uamuzi huo kwa kuwa ushauri wake kuhusiana na suala la Tegeta Escrow haukueleweka.

Taliban yafanya Shambulio kwenye shule Pakistan, waathirika wakubwa ni watoto

Takriban watu 126, wameuwawa wengi wao wakiwa ni watoto na wengine kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia Shule moja inayomilikiwa na Jeshi Kaskazini Magharibi mwa Pakistan. Wakuu katika jimbo la Peshawar wamesema kwamba wapiganaji wapatao sita wenye silaha waliingia katika Shule hiyo yenye na Wanafunzi 500. Maafisa usalama wa Pakistan kwa sasa wamezingira jumba hilo huku milio ya risasi ikisikika, huku jitihada za kuwaokoa wanafunzi hao zikiendelea. Waziri mku wa Pakistan amesema watu zaidi ya 80 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa ni watoto chini ya miaka 12 na 16, huku kwa upande wa wapiganaji wawili wa Talebanwakiuawa ikiwemo mmoja aliyejiua mwenyewe ambapo shambulio hilo likisemekana kuwa ni la kulipiza kisasi cha Wataleban waliouawa na Vikosi vya Usalama vya Jeshi la Pakistan.
 
Blogger Templates