Tuesday, December 16, 2014
Taliban yafanya Shambulio kwenye shule Pakistan, waathirika wakubwa ni watoto
Takriban watu 126, wameuwawa wengi wao wakiwa ni watoto na wengine
kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia Shule moja
inayomilikiwa na Jeshi Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.
Wakuu katika jimbo la Peshawar wamesema kwamba wapiganaji wapatao sita
wenye silaha waliingia katika Shule hiyo yenye na Wanafunzi 500.
Maafisa usalama wa Pakistan kwa sasa wamezingira jumba hilo huku milio
ya risasi ikisikika, huku jitihada za kuwaokoa wanafunzi hao
zikiendelea.
Waziri mku wa Pakistan amesema watu zaidi ya 80 wamejeruhiwa wengi wao
wakiwa ni watoto chini ya miaka 12 na 16, huku kwa upande wa wapiganaji
wawili wa Talebanwakiuawa ikiwemo mmoja aliyejiua mwenyewe ambapo
shambulio hilo likisemekana kuwa ni la kulipiza kisasi cha Wataleban
waliouawa na Vikosi vya Usalama vya Jeshi la Pakistan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment